TECHNOLOGY

Ford kuuza magari ya kusoma ishara




Kampuni ya magari ya Ford itaanza kuuza magari ambayo yatakuwa na uwezo wa kusoma ishara za barabarani na kurekebisha mwendo wake ili kuhakikisha kuwa gari haliendi kwa kasi.
Teknolojia hiyo inatumika kwa kutumia usukani wa gari na inaweza kutolewa kwa kutumia kikanyagio cha kuendesha gari iwapo dereva atakanyaga kikanyagio hicho cha mafuta kwa nguvu.
Kampuni hiyo ya magari inapendekeza kwamba kifaa hicho kitawasaidia madereva kukwepa kulipishwa faini na pia huenda kikapunguza idadi ya ajali.

Hatahivyo mtaalam mmoja amesema kuwa teknolojia hiyo itatumika kwa mda mfupi.
''Kuna mpango wa kudhibiti kasi ya gari lako kupitia kifaa kitakachowekwa katika kompyuta ya gari hilo na kudhibitiwa kutoka eneo hilo,badala ya kutafuta kifaa cha kusoma ishara za barabarani'',alisema Paul Newton mshauri wa maswala ya magari.

''Hii ni miongoni mwa mikakati itakayounganisha mifumo ya magari ,na kuyafanya magari kuonya magari mengine yalio nyuma yao iwapo yanataka kupunguza mwendo ikiwa ni kati ya mipango ya kutengeza magari yanayoweza kujiendesha.
Post a Comment

Post a Comment